WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 13 June 2014

MAELFU WAJITOKEZA KUFANYA USAILI NAFASI YA MKAGUZI MSAIDIZI UHAMIAJI, UWANJA WA TAIFA LEO

Sehemu ya waombaji zaidi ya 10,000 wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi, Idara ya Uhamiaji wakifanya usaili wa awali wa kuandika ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ajili ya kujaza nafasi 70 za kazi ambazo zinahitajika katika Idara hiyo. Usaili huo uliongozwa na Maafisa Utumishi wa wizara hiyo, umefanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja waliofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Afisa Utumishi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Penina Isamuyo akigawa makaratasi ya mitihani kwa waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi, Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya kufanya usaili wa awali wa kuandika.  Zaidi ya waombaji 10,000 walifanya usaili huo Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja watakaofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Afisa Utumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwanamridu Jumaa (aliyevaa kiraia) na askari Magereza wakiwa wamebeba maboksi yenye makaratasi ya mitihani ya usaili iliyofanywa na zaidi ya waombaji 10,000 Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo. Baada ya wiki moja waombaji waliofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akisimamia usahihishaji wa mitihani ya usaili ya waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji inayosahihishwa na Maafisa Utumishi wa wizara na askari Magereza. Zaidi ya waombaji 10,000 wamefanya usaili wa awali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kugombea nafasi 70 zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akisimamia usahihishaji wa mitihani ya usaili ya waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji inayosahihishwa na Maafisa Utumishi wa wizara na askari Magereza. Zaidi ya waombaji 10,000 wamefanya usaili wa awali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kugombea nafasi 70 zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo.

Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lubert Fransis (kulia) na Mwanamridu Jumaa wakipanga maboksi kwa ajili ya kuhifadhia makaratasi ya mitihani ya usaili. Zaidi ya waombaji 10,000 walifanya usaili wa awali Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja waliofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (kushoto) akiwa na Meneja wa Uwanja wa Taifa, Rish Moses wakati wa usaili wa waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji.  Zaidi ya waombaji 10,000 wamefanya usaili wa awali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kugombea nafasi 70 zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 
  PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHINo comments:

Post a comment