WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 5 June 2015

WAZIRI CHIKAWE AONGOZA KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KAMISHNA MKUU MSTAAFU JESHI LA MAGEREZA, ONEL MALISA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akiweka saini katika daftari la rambirambi kwenye msiba wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa wakati wa ibada iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimpa pole mke wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akiweka saini katika daftari la rambirambi kwenye msiba wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa wakati wa ibada iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri nchini (KKKT), Usharika wa Kinyerezi, Manford Kijalo akiwaongoza askari waliobeba mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa wakati mwili huo ukiwasili katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akitoa heshima wakati mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa ulipokuwa unawasili katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Probesheni na Huduma kwa Jamii, Aloyce Msika akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa jeshi hilo, Onel Malisa wakati mwili huo ukipelekwa ndani ya gari kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi. Tukio la kuuga mwili huo lilifanyika  katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a comment