WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 11 August 2014

MORAVIAN WAMPONGEZA WAZIRI CHIKAWE

HALMASHAURI Kuu ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Misheni Mashariki, imempongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe baada ya kutoa tamko la kukemea ubinafsi na uroho wa madaraka kwa baadhi ya viongozi wa kanisa hilo nchini. Katibu Mkuu wa kanisa hilo katika misheni hiyo, Mchungaji Emmaus Mwamakula alitoa kauli hiyo juzi wakati wa mkutano baina ya halmashauri hiyo na wanahabari uliofanyika Dar es Salaam juzi uliolenga kutolea ufafanuzi kuhusu wachungaji 18 kuvuliwa uchungaji na Askofu Lusekelo Mwakafwila. Aliongeza kuwa halmashauri kuu inapenda jamii ifahamu Askofu Mwakafwila wa Jimbo la Kusini Rungwe na Askofu Alinikisa Cheyo wa Jimbo la Kusini Magharibi Mbeya wapo nyuma ya mgogoro wa Jimbo la Kusini Magharibi Mbeya. CHANZO: Gazeti la Jamboleo, Uk. 3.

No comments:

Post a comment