WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Thursday, 23 February 2017

KAMISHNA WA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI MASAUNI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Kamishna wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, wakati Kamishna huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kupambana na dawa za kulenya nchini.
Kamishna wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga (kushoto), akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati Kamishna huyo alipomtembelea Masauni ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kupambana na dawa za kulenya nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkaribisha Kamishna wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusu kupambana na dawa za kulevya nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Thursday, 16 February 2017

KATIBU MKUU RWEGASIRA: UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA MSUMBIJI BADO UPO IMARA, AWATAKA WATANZANA KUFUATA SHERIA ZA UHAMIAJI NCHI WANAZOISHI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Watanzania wanaorudishwa nchini kutoka Msumbiji. Rwegasira amesema Uhusiano kati ya Tanzania na Msumbiji unaendelea kuimarika kila siku, hivyo aliwataka Watanzania wafuate Sheria za Uhamiaji za nchi hiyo kwani zoezi linalofanyika nchini humo halijawalenga Watanzania pekee bali raia wote wanaoishi na kufanya kazi bila kufuata taratibu za kisheria nchini humo. Aidha, amewataka wananchi kutolikuza tukio hilo bila sababu za msingi. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Watanzania wanaorudishwa nchini kutoka Msumbiji. Rwegasira amesema Uhusiano kati ya Tanzania na Msumbiji unaendelea kuimarika kila siku, hivyo aliwataka Watanzania wafuate Sheria za Uhamiaji za nchi hiyo kwani zoezi linalofanyika nchini humo halijawalenga Watanzania pekee bali raia wote wanaoishi na kufanya kazi bila kufuata taratibu za kisheria nchini humo. Aidha, amewataka wananchi kutolikuza tukio hilo bila sababu za msingi. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. 

Thursday, 2 February 2017

UHAMIAJI KUTOA PASIPOTI KWA SIKU TANO KUANZIA SASA, NAIBU KATIBU MKUU SIMBA AZINDUA MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA, JIJINI DAR LEO

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Idara ya Uhamiaji. Mkataba huo ambao unalenga kuimarisha huduma mbalimbali za Idara hiyo pia umeelekeza kuanzia sasa Hati za Kusafiria (Pasipoti) zitatolewa kwa siku tano za kazi kwa watakaoomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akizungumza na wananchi (wateja) waliofika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji kabla ya Balozi huyo hajazindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ulioandaliwa na Idara hiyo. Simba alisema Mkataba huo unalenga kuimarisha huduma za Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (aliyevaa tai) akimsikiliza mteja aliyefika kupata huduma ya Pasipoti Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam mara baada ya Balozi huyo kuwauliza maswali wateja waliofika ofisini hapo. Hata hivyo, wateja hao walisema wanapewa huduma nzuri na maafisa wa Idara hiyo. Balozi Simba alizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ambao unalenga kuimarisha utoaji wa huduma bora katika Idara hiyo. Katikati ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akizungumza na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini kabla ya Balozi huyo kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ulioandaliwa na Idara hiyo ambao unalenga kuboresha zaidi huduma zitolewazo na Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto (upande wa pili) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati), akimsikiliza Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli alipokuwa anatoa maelezo mafupi jinsi Watendaji wa Idara yake walivyouandaa Mkataba wa Huduma kwa Mteja ambao Balozi huyo aliuzindua Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Mkataba huo unalenga kuboresha zaidi huduma zitolewazo na Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia), akimkabidhi Vitabu vya Mkataba wa Huduma kwa Mteja Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara Uhamiaji, Victoria Lembeli mara baada ya Naibu Katibu Mkuu huyo kuzindua Mkataba huo katika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Mkataba huyo unaelekeza kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.