WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Thursday 31 March 2016

WAZIRI KITWANGA, VIONGOZI WAKUU UHAMIAJI NA JESHI LA ZIMAMOTO WAFANYA KIKAO CHA MAPITIO YA RASIMU YA BAJETI KWA MWAKA 2016/17

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Wizara yake ya Mwaka 2016/17 kwa upande wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Idara ya Uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo, kilijumuisha Viongozi Wakuu wa Taasisi hizo pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimsikiliza Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (kulia) wakati alipokuwa anatoa taarifa yake katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 kwa Idara ya Uhamiaji kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kikao hicho kilijumuisha Viongozi Wakuu wa Uhamiaji na Wakuu wa Idara ya Wizara hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akiwafafanulia jambo Viongozi Wakuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Wakuu wa Idara ya Wizara yake katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 kwa Jeshi hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wa tatu kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Rogatius Kipali.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kulia) akizungumza na Viongozi Wakuu wa Idara ya Uhamiaji katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 ya Wizara yake. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo, pia kilihudhuriwa na Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akifuatiwa na Mrakibu Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji, Joseph Mtenga.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a Comment