Sehemu ya waombaji zaidi ya 10,000 wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi, Idara
ya Uhamiaji wakifanya usaili wa awali wa kuandika ulioandaliwa na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ajili ya kujaza nafasi 70 za kazi ambazo
zinahitajika katika Idara hiyo. Usaili huo uliongozwa na Maafisa Utumishi wa
wizara hiyo, umefanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada
ya wiki moja waliofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Afisa Utumishi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Penina Isamuyo akigawa
makaratasi ya mitihani kwa waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi, Idara ya
Uhamiaji kwa ajili ya kufanya usaili wa awali wa kuandika. Zaidi ya waombaji 10,000 walifanya usaili huo
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja watakaofaulu
vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Afisa Utumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwanamridu Jumaa
(aliyevaa kiraia) na askari Magereza wakiwa wamebeba maboksi yenye makaratasi
ya mitihani ya usaili iliyofanywa na zaidi ya waombaji 10,000 Uwanja wa Taifa,
jijini Dar es Salaam leo. Baada ya wiki moja waombaji waliofaulu vizuri
wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Lilian Mapfa akisimamia usahihishaji wa mitihani ya usaili ya waombaji wa
nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji inayosahihishwa na Maafisa
Utumishi wa wizara na askari Magereza. Zaidi ya waombaji 10,000 wamefanya
usaili wa awali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kugombea nafasi
70 zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo.

Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lubert Fransis (kulia) na
Mwanamridu Jumaa wakipanga maboksi kwa ajili ya kuhifadhia makaratasi ya
mitihani ya usaili. Zaidi ya waombaji 10,000 walifanya usaili wa awali Uwanja
wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja waliofaulu vizuri
wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Lilian Mapfa (kushoto) akiwa na Meneja wa Uwanja wa Taifa, Rish Moses
wakati wa usaili wa waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji.
Zaidi ya waombaji 10,000 wamefanya
usaili wa awali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kugombea nafasi
70 zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment