WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Thursday, 12 June 2014

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAKUTANA KUANDAA MPANGO KAZI NA MPANGO WA MANUNUZI KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015


Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (aliyevaa tai) wakiwa katika Kikao cha kuandaa Mpango Kazi na Mpango wa Manunuzi kwa mwaka wa fedha 2014/15 kinachofanyika katika Chuo cha Kanda cha Uhamiaji mjini Moshi. Aliyesimama ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi wa Wizara hiyo, Manyama Mapesi. Kikao hicho kinawajumuisha Watendaji Wakuu wa Idara za Wizara, Maafisa Bajeti pamoja na Maafisa Manunuzi.Baadhi ya Viongozi wa Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wanaohudhuria kikao cha kuandaa Mpango Kazi na Mpango wa Manunuzi wa Wizara hiyo katika Chuo cha Kanda cha Uhamiaji mjini  Moshi, (toka kulia) Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga, Kamishna wa Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi, Clodwig Mtweve, Kamishna wa Urekebishaji wa Jeshi la Magereza, Deonice Chamulesile na Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Juma Mohammed. 

PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment