Mnamo
tarehe 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani,watu
wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi
Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu
kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada.
Cha
kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika kwa jina
la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha aina
ya SMG ikiwa na risasi 30.
Ndipo
walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya
pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka
kusikojulikana.
Askari
Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya
wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE amejeruhiwa mgongoni kwa
risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia.
Mgambo
Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana
mateke na kujeruhiwa mbavuni. Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa
Hospitali hiyo aitwaye VERONICA MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki
akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili
kwa matibabu ya kina.
Kazi
ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe makini sana na stahili hii ya ujambazi;
HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni kuwapata watuhumiwa wote na
silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali mkoa ulipo, taarifa za haraka
tunatarajia kupata toka kwako kuhusiana na wahusika wa tukio hili.
SOURCE: MICHUZI
BLOG
No comments:
Post a Comment