Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Inspekta Jenerali
wa Polisi (IGP) Ernest Mangu (kushoto), Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester
Ambokile (wanne kushoto) wakipokea taarifa kuhusu Mfumo wa Ufuatiliaji wa Mienendo
ya Watu (Public Surveilance Sytem (Global eye) kutoka kwa Mtaalam wa Kampuni ya Telecom ya
nchini China. Waziri Chikawe na ujumbe wake wapo jijini Beijing, China kwa
ziara ya kikazi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimsikiliza kwa makini
Mwenyekiti wa Kampuni ya Kutoa Huduma ya Mawasiliano nchini China, Li Ping
alipokuwa akimfafanulia masuala mbalimbali ya mawasiliano yanayofanywa na Kampuni
yake. Waziri Chikawe yupo jijini Beijing nchini humo na Inspekta Jenerali wa Polisi
(IGP) Ernest Mangu, Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile kwa
ajili ya ziara ya kikazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Inspekta Jenerali
wa Polisi (IGP) Ernest Mangu, Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester
Ambokile wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kutoa Huduma
ya Mawasiliano nchini China, Li Ping. Waziri Chikawe na ujumbe wake wapo jijini
Beijing, China kwa ziara ya kikazi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment