RAIA wa Nigeria,
Anthony Ifeanyichukwa Okafor (52), amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere akidaiwa kumeza kete 100 za dawa za kulevya aina ya cocaine
ambazo thamani yake bado haijafahamika.
Tukio hilo limetokea
takribani siku 22 baada ya raia mwingine wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65)
kuvunja rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya katika
uwanja huo.
Cole alikamatwa
Jumatatu ya Mei 19, mwaka huu saa tisa alasiri akijiandaa kwenda Paris,
Ufaransa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, akiwa amemeza kete 82 aina
ya heroini zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi zinazofanana na ganda la
sigara, ambazo si rahisi kuonekana katika mitambo.
Mkuu wa Kitengo cha
Polisi cha Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alisema jana
kuwa amefika nchini kumfuata rafiki yake wa kike aliyekutana naye Hong Kong,
China na baadaye Douala, Cameroon.
Nzowa alisema mtuhumiwa
huyo alisema rafiki yake huyo wa Tanzania ni mpenzi wake na wako pamoja katika
kazi hiyo.
Kamanda wa Polisi wa
Uwanja wa Ndege, Hamisi Selemani alisema wauzaji wa dawa hizo siku hizi
wamegundua mtindo mpya wa kuwatumia watu wazima ili wasigundulike kutokana na
mwonekano wao.
No comments:
Post a Comment