WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 6 June 2016

SERIKALI YA JAPAN YATOA MSAADA WA MAGARI TISA KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (katikati) na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshiba (kushoto) wakikata utepe ikiwa ishara ya makabidhiano ya magari matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini. Magari hayo yamekabidhiwa nje ya Jengo la Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia anayepiga makofi ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Thobias Andengenye.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akitoa hotuba fupi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuishukuru Serikali ya Japan kwa kuisadia wizara yake kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji magari tisa kwa ajili ya kazi ya kuzima moto na uokoaji nchini. Wa pili kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshiba akifuatiwa na Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Thobias Andengenye. Wa pili kulia ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, Rogatus Kipali na Kamishna Msaidizi, Fikiri Salla. Tukio hilo lilifanyika nje ya Jengo la Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Thobias Andengenye akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi ili aweze kuzungumza na baadaye kukabidhiwa magari matano ya kuzima moto na uokoaji. Magari hayo yametolewa na Serikali ya Japan kupitia balozi wake nchini, Masaharu Yoshiba. Tukio hilo la makabidhiano lilifanyika nje ya Jengo la Wizara hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (kushoto) akimkabidhi zawadi Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshiba, mara baada ya Balozi huyo kuikabidhi Wizara hiyo msaada wa magari tisa ya kuzima moto na uokoaji. Tukio la makabidhiano ya magari hayo lilifanyika nje ya Jengo la Wizara, jijini Dar es Salaam leo.
Wakuu wa Idara ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wageni waalikwa, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake kabla ya Serikali ya Japan kutoa msaada wa magari tisa ya kuzima moto na uokoaji. Tukio hilo lilifanyika nje ya Jengo la Wizara, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Andengenye aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaada mkubwa ambao wameutoa kwa Jeshi lake.
 
Sehemu ya magari tisa yaliyokabidhiwa na Balozi wa Japan, Masaharu Yoshiba kwa niaba ya Serikali yake yakiwa nje ya Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Magari hayo yaliyotolewa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yalipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara hiyo, Haji Janabi, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment