WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Sunday 24 August 2014

KAMATI YA KUWAHOJI WAOMBA HIFADHI (NEC) YAANZA KAZI KAMBI YA WAKIMBIZI NYARUGUSU, KIGOMA


Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kuhoji Waomba Hifadhi (NEC), Faraja Nchimbi (katikati-meza kuu) akiwa na wajumbe wa Kamati hiyo wakati walipokuwa wanawahoji waomba hifadhi (hawapo pichani) katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Waombaji hao wanatoka nchi mbalimbali ambapo wengi wao ni Wakongo. Zaidi ya waomba hifadhi 300 wanahojiwa na Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Taasisi nane za Serikali ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP), Idara ya Wakimbizi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Inspekta Jererali wa Polisi, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Shirika la Kimataifa ya Kuhudumia Wakimbizi ambao ni waangalizi wa tukio hilo.

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kuhoji Waomba Hifadhi (NEC), Faraja Nchimbi (watatu kushoto), Katibu wa Kamati hiyo, Philo Nombo (watatu kulia) ambaye anamwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo baada ya kuwahoji waomba hifadhi katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Waombaji hao wanatoka nchi mbalimbali ambapo wengi wao wanatoka nchini Kongo. Zaidi ya waomba hifadhi 300 wanaendelea kuhojiwa na Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Taasisi nane za Serikali ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP), Idara ya Wakimbizi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Inspekta Jererali wa Polisi, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Shirika la Kimataifa ya Kuhudumia Wakimbizi ambao ni waangalizi wa tukio hilo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment