WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday 3 August 2015

RAIS KIKWETE AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA JIJINI TANGA LEO

Mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa jijini Tanga leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Endesha Salama Okoa Maisha”. Katika hotuba yake, Rais Kikwete aliwataka Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani wabadili mfumo walionao kutoka Analogi kwenda Digitali ili mfumo huo uweze kupunguza rushwa pamoja na ajali nchini.

Washiriki wa maonesho wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Kiwanja cha Tangamano, jijini Tanga leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Endesha Salama Okoa Maisha”. Katika hotuba yake, Rais Kikwete ambaye ndiye aliyefungua maandamano maadhimisho hayo, aliwataka Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani wabadili mfumo walionao kutoka Analogi kwenda Digitali ili mfumo huo uweze kupunguza rushwa pamoja na ajali nchini. 

Washiriki wa maonesho ambao ni wanafunzi wa shule za msingi jijini Tanga wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe usemao ‘Sote tuna Haki ya Kutumia Barabara’, kundi hilo la wanafunzi  hao ambao ni moja ya makundi ya waandamanaji wakiwa wanapita mbele ya jukwaa la mgeni rasmi, Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa wiki hiyo. Rais Kikwete ambaye ndiye aliyefungua maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama jijini humo, aliwataka Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani wabadili mfumo walionao kutoka Analogi kwenda Digitali ili mfumo huo uweze kupunguza rushwa pamoja na ajali nchini. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani nchini,  Pereira Ame Silima akitoa hotuba yake kabla ya kumkabirisha mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete kuja kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambapo kwa mwaka huu imebeba kauli mbiu ya “Endesha Salama Okoa Maisha”. Katika hotuba yake, Silima aliwataka madereva nchini kufuata sheria za barabarani ili waweze kuepuka ajali ambazo nyingi zinasababishwa na uzembe wao.

Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika sanamu lenye kuonyesha mtu akiwa anavuka barabara katika eneo la kivuko cha waenda kwa miguu katika Banda la Maonesho la Usalama Barabarani wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliozinduliwa na Rais Kikwete, jijini Tanga leo. Katika hotuba yake kabla ya kuyazindua maadhimisho hayo, Rais Kikwete aliwataka Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani wabadili mfumo walionao kutoka Analogi kwenda Digitali ili mfumo huo uweze kupunguza rushwa pamoja na ajali nchini. Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kaimu Kamishna wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamedi Mpinga. Kushoto ni Trafiki kutoka Makao Makuu Dar es Salaam, Meja Enock Machunde.

Wananchi mbalimbali na wageni waalikwa wakiwa katika harakati ya kuingia katika mabanda mbalimbali katika Kiwanja cha Tangamano, jijini Tanga mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani jijini humo. Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo ni ‘Endesha Salama Okoa Maisha’. Rais Kikwete katika hotuba yake ya ufunguzi amewataka Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani wabadili mfumo walionao kutoka Analogi kwenda Digitali ili mfumo huo uweze kupunguza rushwa pamoja na ajali nchini.

Rais Jakaya Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua reflector mpya za kubandikwa kwenye magari nchini ili ziweze kuzuia ajali. Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na kushoto ni Kaimu Kamishna wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Jeshi la Polisi, Mohamedi Mpinga. Rais Kikwete alizindua Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa inafanya katika Kiwanja cha Tangamano, jijini Tanga. Katika hotuba yake, Rais Kikwete aliwataka Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani wabadili mfumo walionao kutoka Analogi kwenda Digitali ili mfumo huo uweze kupunguza rushwa pamoja na ajali nchini.

Waendesha pikipiki (bodaboda) pia walishiriki kikamilifu katika uzinduzi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Kiwanja cha Tangamano jijini Tanga leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Endesha Salama Okoa Maisha.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment