WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wednesday 9 September 2015

ZOEZI LA KUWAPOKEA WAKIMBIZI TOKA BURUNDI LAENDELEA VIZURI KAMBI YA NYARUGUSU




Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Fredrick Nsajile akizungumza na wakimbizi waliopo katika mpango wa kuhamishiwa kwenye Kambi za Nduta, Mtendeli na Karago.Wakimbizi hao waliopokelewa kutoka nchini Burundi hivi karibuni kwa sasa wanahifadhiwa kwa muda katika Kambi ya Nyarugusu.

Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Kukimana Dafroza (katikati), akifuma kikapu katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa katika kambi nyingine. Wengine ni Mkabanura Eviline (kushoto) na Niragira Dafroza (kulia).

Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wakichota maji katika moja ya vituo vya maji vilivyowekwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu Mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda.  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) ina mpango wa kuwahamishia katika kambi za Karago, Mtendeli na Nduta ili kupunguza msongamano uliopo katika Kambi ya Nyarugusu.
Mkimbizi Ntirampeba Acquilina aliyeko katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu akiandaa mihogo ya kuwauzia wakimbizi wenzake wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mkimbizi Haverimana Ejide (kulia) na mkewe Kugimana Evona pamoja na watoto wao wakipata chakula cha mchana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa maeneo mengine ili kupunguza msongamano uliopo katika kambi ya Nyarugusu.
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Jacqueline Elulu (mwenye mtoto), akisubiri kupata huduma ya afya katika kituo cha Red Cross kinachotoa huduma za afya kwa wakimbizi walioko katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.




No comments:

Post a Comment