WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday 18 March 2016

WAZIRI KITWANGA ATEMBEA MITAANI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA PEMBA, ATEMBELEA MSITU WA NGEZI NA KUGUNDUA HAKUNA WAKIMBIZI WOWOTE


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wa pili kulia) akitembea mitaani eneo la Chake Chake Pemba, Zanzibar kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu usalama wao katika kipindi cha uchaguzi kisiwani humo. Waziri Kitwanga ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdullah (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman (wapili kushoto aliyevaa kaunda suti) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kusini Pemba, Ahmed Khalid Abdulla (kushoto, aliyevaa tai. Kitwanga aliridhishwa na juhudi za kuimarisha ulinzi katika kisiwa hicho.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuuzunguka msitu wa Taifa wa Ngezi, uliopo Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba ambao baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar walisambaza taarifa za uongo kuwa kuna wakimbizi wamejificha katika msitu huo baada ya kukimbia vurugu kisiwani humo. Hata hivyo hakuna mkimbizi yeyote aliyekuwepo katika msitu huo na wananchi wapo katika makazi yao wakiendelea na shughuli zao za kujitafutia kipato. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nasri.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na wauza nguo wa Soko Kuu la mjini Chake Chake, Pemba. Wananchi hao walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida bila wasiwasi wowote. Waziri Kitwanga pia alisikiliza maoni ya wananchi hao kuhusu uchaguzi mkuu na kuridhishwa na juhudi za kuimarisha ulinzi katika kisiwa hicho.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, mjini Chake Chake, Pemba, kuhusu masuala mbalimbali ya uimarishaji ulinzi katika kipindi cha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 20, 2016. Kushoto meza kuu ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdullah na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akimuuliza swali Mkazi wa Wawi, Chake Chake Pemba, bibi Zabibu Mohamedi, wakati Waziri huyo alipokuwa anatembea mitaani kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 20, 2016. Hata hivyo wananchi hao walimuahkikishia kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika siku hiyo ya uchaguzi.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akiwahoji wafanyakazi wa Bandari Kuu ya Pemba kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Machi 20, 2016. Wafanyakazi hao walimuhakikishia kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo na pia wananchi hao wapo salama na wanaendelea na shughuli zao zakujipatia kipato za kila siku.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akiwauliza maswali wananchi wa mjini Chake Chake, Pemba kuhusu jinsi walivyojiandaa na uchaguzi wa Machi 20, 2016 na kutoa maoni yao kama kuna tatizo lolote. Hata hivyo wananchi hao walimuambia Waziri Kitwanga wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, hakuna vitisho vyovyote katika eneo lao. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a Comment