Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir
Minja(kushoto) akikabidhi cheti kwa Mfanyakazi bora kwa Mwaka 2014, Bw.
John Chacha(kulia) ambaye ni Mhudumu wa Ofisi daraja la pili katika
Ofisi ya Magereza Mkoani Mwanza. Zawadi kwa Wafanyakazi raia wa Jeshi la
Magereza hutolewa kutokana na utendaji mzuri wa kazi pamoja na nidhamu
kazini. Hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa Watumishi hao imefanyika leo
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi Bora wa Jeshi la Magereza kwa Mwaka 2014 ambao wamekabidhiwa
zawadi zao leo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John
Casmir Minja(hayupo pichani) wakisikiliza kwa makini wakati Mwenyekiti
wa TUGHE Tawi la Jeshi la Magereza alipokuwa akitoa neno la shukrani kwa
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza katika hafla fupi ya kukabidhi
zawadi kwa Wafanyakazi Bora wa Jeshi la Magereza, leo Julai 3, 2014
Jijini Dar es Salaam(katikati) ni Mhudumu wa Ofisi daraja la Pili, Bw.
John Chacha kutoka Ofisi ya Magereza Mkoani Mwanza.
Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza waliohudhuria hafla fupi ya
kukabidhi zawadi kwa Wafanyakazi bora wa Jeshi la Magereza(hawapo
pichani) wakifurahia jambo wakati Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Jeshi la
Magereza alipokuwa akitoa neno fupi la shukrani kwa Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Magereza. Kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la
Magereza, Gaston Sanga(kushoto) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza, Clement Keenja.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa
nasaha zake fupi katika hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa Wafanyakazi
Bora raia wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kwa Mwaka 2014. Hafla
hiyo fupi imefanyika leo Julai 3, 2014 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Jeshi la Magereza, Bw. Sedumba
Katenda(katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na
Watumishi raia wa Jeshi la Magereza mara tu baada ya hafla fupi ya
kukabidhiwa zawadi kwa Wafanyakazi bora wa Jeshi la Magereza. Hafla hiyo
imefanyika leo Julai 3, 2014 katika Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi
la Magereza Nchini(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment