WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 24 October 2014

WAZIRI CHIKAWE AMKABIDHI MKUU WA WILAYA NACHINGWEA MABATI 2000 KWA AJILI YA UJENZI WA MAABARA SHULE ZA SEKONDARI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo mabati 2000 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara za Shule 20 za Sekondari wilayani humo. Waziri Chikawe ametoa msaada huo baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa agizo kwa kila mwana jamii nchini kuchangia ujenzi wa maabara katika shule za Kata nchini. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Abdalla Chikawe (wapili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Valery Kwembe wakiyaangalia msaada wa mabati yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo kwa ajili ya kuzisaidia Shule za Sekondari za Kata kwa ajili ya ujenzi wa maabara. Makabidhiano ya mabati hayo 2000 yalifanyika nyumbani kwa Waziri Chikawe mjini Nachingwea leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a Comment