WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Thursday 11 December 2014

BALOZI WA MAREKANI AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akimkaribisha Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (kulia) pamoja na maofisa wa ubalozi huo, ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe na Balozi huyo walizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya Balozi huyo nchini.
Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ubalozi wa Marekani na wizara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya Balozi huyo nchini. Balozi Childress alimtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment