WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 2 September 2014

KIKAO KAZI CHA WATENDAJI WA SHIRIKA LA MAGEREZA, GEPF MKOANI MOROGORO

Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine (kushoto) akiteta jambo na Watendaji Waandamizi wa Shirika la Magereza na GEPF kabla ya kutembelea katika eneo la Kihonda, Morogoro ambapo mradi wa Majengo ya vitega uchumi kwa ubia kati ya Shirika la Magereza na GEPF utakapojengwa(wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, Bw. Festo Fute(wa pili kulia) ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga.
Watendaji Wakuu wa Shirika la Magereza, GEPF na Wataalam Washauri wakiendelea na Kikao kazi katika eneo la Kihonda, Mkoani Morogoro ambapo mradi wa Majengo ya vitega uchumi utakapojengwa kama inavyoonekana katika picha.
Msanifu wa Majengo toka Kampuni CONS AFRIKA ya Jijini Dar es Salaam, Bw. Henry Mwoleka(wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo muhimu wakati Watendaji wa Shirika la Magereza, GEPF na Wataalam washauri walipotembelea eneo la Uwekezaji la Kihonda, Mkoani Morogoro ambapo mradi wa Majengo ya vitega uchumi utafanyika. Timu hiyo ya Wataalam imeendelea na Kikao chake leo Agosti 1, 2014 Mkoani Morogoro(wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine(wa pili kushoto) ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga wakisikiliza maelezo ya Msanifu Majengo wa Kampuni ya CONS AFRIKA ya Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Gereza Kihonda, Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Ben Mwansasu akiwaonesha eneo la Uwekezaji Watendaji Wandamizi wa GEPF na Wataalam washauri walipotembelea eneo hilo leo Agosti 1, 2014 Mkoani Morogoro. Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza limeingia Makubaliano ya ubia na Mfuko wa Jamii wa GEPF katika miradi ya ujenzi wa Majengo ya vitega uchumi katika eneo la Karanga, Kilimanjaro na Kihonda Mkoani Morogoro.

Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Waandamizi wa Shirika la Magereza, GEPF na Wataalam washauri mara tu baada ya kikao kazi cha kupitia na kuangalia maeneo ya Uwekezaji katika miradi ya vitega uchumi utakaofanyika. Kikao hicho kimeendelea leo Agosti 1, 2014 Mkoani Morogoro. (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

GARI LA ABIRIA AINA YA HIACE LAKAMATWA NA VIPANDE 70 VYA NONDO MALI YA WIZI NA WATUHUMIWA SITA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
                                                                     
PRESS RELEASE
02/09/2014



GARI LA ABIRIA AINA YA HIACE LAKAMATWA NA VIPANDE 70 VYA NONDO MALI YA WIZI NA WATUHUMIWA SITA 

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam limekamata gari namba T 784 AFA, Toyota HIACE likiwa na vipande 70 vya Nondo. Gari hili limekamatwa tarehe 29/08/2014, majira ya saa saba usiku maeneo ya barabara ya Ferry Kimbiji baada ya askari waliokuwa doria kupokea taarifa kuwepo kwa gari hilo lililobeba mali hizo idhaniwayo kuwa ni ya wizi.
Aidha taarifa za awali zinaonyesha kuwa mali hiyo imeibwa katika maeneo mbalimbali ya ujenzi unaoendelea huko maeneo ya Kimbiji na Somangira Kigamboni Mkoa wa Kipolisi Temeke.
Watuhumiwa waliokamatwa ni kama ifuatavyo:

1.    SHIJA S/O MGENI, Miaka 22, Mkazi wa Mbagala
2.    ALLY S/O MANGILUNGI, Miaka 18, Mkazi wa Kurasini.
3.    NASSORO S/O RAMADHANI, Miaka 35, Mkazi wa Mbagala Charambe.
4.    RAJABU S/O HASSAN, Miaka 32, Mkazi wa Mbagala Charambe.
5.    SAMSON S/O MDINGI, Miaka 27, Mkazi wa Kurasini.
6.    AMINI S/O SAID, Miaka 15, Mkazi wa Kurasini. 

Nawaomba wananchi waendelee kulisaidia Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhakika zitakazosaidia kuwakamata wahalifu kama hawa wanaodhoofisha jitihada za maendeleo kwa wawekezaji na Serikali kwa kupora vifaa vya miundombinu ya ujenzi na vitu kama hivi.

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM