WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 24 October 2014

WAZIRI CHIKAWE AIBOMOA NGOME YA CHADEMA NACHINGWEA, VIGOGO, WANACHAMA WAO WARUDI KWA KISHINDO CCM

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (watano kulia waliosimama) akiwa na wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kukikimbia chao cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Wananchama hao 23 wakiongozwa na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa chama hicho wilayani Nachingwea, Manufreda Malenga (watano kushoto waliosimama) walifanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akimkabidhi kadi ya CCM, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani humo, Manufreda Mathias Malenga. Kiongozi huyo pamoja na wanachama wengine 22 wa chama hicho wamekikimbia chao chao na kujiunga na CCM na kufanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akimpongeza Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema Kata ya Mtua, Habibu Oswadi (kushoto) baada ya kukabidhi kadi ya chama chake. Kiongozi huyo wa Kata pamoja na wanachama wengine 22 wa chama hicho wamekikimbia chao chao na kujiunga na CCM na kufanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Abdalla Chikawe (wapili kulia kwa mgeni rasmi).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na Viongozi wa CCM Wilaya, Kata pamoja na wananchi waliofurika katika Uwanja uliopo jirani na Ofisi za CCM Kata ya Mtua katika sherehe kubwa ya kuwapokea viongozi wawili na wanachama 21 wa Chadema waliojiunga na CCM wilayani humo.   Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi ambapo aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo.
Mwanachama mpya wa CCM ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Nachingwea, Manufreda Mathias Malenga akizungumza kwa hisia baada ya kupewa nafasi kueleza furaha yake baada ya kukabidhi kadi ya Chadema na kupewa kadi pamoja na sare za CCM. Malenga aliwashukuru Viongozi na wanachama wa CCM kwa kumkaribisha katika chama hicho na kuahidi kutoa ushirikiano wake ndani ya chama hicho. Kiongozi huyo pamoja na wanachama wengine 22 wa chama hicho wamekikimbia chao chao na kujiunga na CCM na kufanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati meza kuu) alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


WAZIRI CHIKAWE AMKABIDHI MKUU WA WILAYA NACHINGWEA MABATI 2000 KWA AJILI YA UJENZI WA MAABARA SHULE ZA SEKONDARI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo mabati 2000 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara za Shule 20 za Sekondari wilayani humo. Waziri Chikawe ametoa msaada huo baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa agizo kwa kila mwana jamii nchini kuchangia ujenzi wa maabara katika shule za Kata nchini. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Abdalla Chikawe (wapili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Valery Kwembe wakiyaangalia msaada wa mabati yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo kwa ajili ya kuzisaidia Shule za Sekondari za Kata kwa ajili ya ujenzi wa maabara. Makabidhiano ya mabati hayo 2000 yalifanyika nyumbani kwa Waziri Chikawe mjini Nachingwea leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.