WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 13 January 2015

SERIKALI YAUNDA TIMU KUTEMBELEA MAENEO SUGU YA UTEKAJI, UUAJI ALBINO, YAPIGA MARUFUKU WAPIGA RAMLI NCHINI

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati meza-kuu) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Serikali kuunda timu maalumu ya kutembelea maeneo yaliyosugu kwa utekaji na mauaji ya albino nchini ambapo timu hiyo inatarajiwa kuanza kazi wiki mbili zijazo kwa kuanza na mikoa sugu ya matukio hayo ambayo ni Mwanza, Geita, Simiyu, Tabora na Shinyanga na baadaye itafuata mikoa mingine. Pia Waziri Chikawe katika mkutano huo, alitangaza kupiga marufuku wapiga ramli wote nchini kwa kuwa wanasababisha kuendelea kwa matukio ya kinyama wanayotendewa albino. Hata hivyo, katika mapambano ya kusambaratisha unyanyasaji huo, waziri huyo alitangaza kushirikiana ipasavyo na viongozi wa dini pamoja na mashirika ya kijamii ili kusaidia kutoa elimu kwa wananchi kutokana na uhalifu huo dhidi ya albino. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  

No comments:

Post a Comment