Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe (wapili kushoto-mstari wa pili), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na
Mexico, Liberata Mulamula (nyuma ya waziri) wakimsikiliza kwa makini Rais
Barack Obama (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake katika
Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika
katika Ukumbi wa Loy Henderson wa Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC
nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na
masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa
Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala
mbalimbali ya jinsi ya kupambana na vurugu na
ugaidi dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya
watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu,
hivyo hakuna dini yoyote inayowajibika kwa ugaidi, isipokuwa watu ndio
wanaowajibika kwa vurugu na ugaidi. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
|
No comments:
Post a Comment