Katibu
Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo (RESCA), Bw.
Theoneste Mutsindashyaka (kulia) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi, mashine 2 za kuweka alama silaha,
zilizotolewa na Serikali ya Marekani kupitia Kituo hicho chenye Makao Makuu
yake Jijini Nairobi. Halfa hii
ilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo (RESCA), Bw.
Theoneste Mutsindashyaka (kulia) akitoa maelezo jinsi mashine za kuweka alama silaha zinavyofanya
kazi. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwamini Malemi na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu.
Mashine
za kuweka alama silaha, zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la
Polisi Tanzania. Uwekaji wa alama katika
silaha utasaidia udhibiti wa matumizi ya silaha hapa nchini.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akitoa hotuba
kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe kushukuru
msaada wa mashine zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la Polisi
Tanzania kwa ajili ya kuweka alama silaha.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IJP Ernest Mangu akishukuru kuhusu msaada wa mashine
za kuweka alama silaha zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la Polisi
Tanzania katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi jijini Dar es Salaam. Waliokaa toka
kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi
na Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo,
Bw. Theoneste Mutsindashyaka.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa nne kutoka
kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi,
IJP Ernest Mangu (wa tatu toka kulia) na Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda
cha kushughulikia Silaha Ndogondogo (RECSA) Bw. Theoneste Mutsindashyaka (wa
nne toka kushoto) baada ya hafla ya kupokea mashine za kuweka alama silaha
iliyofanyika katika Makao Makuu ya Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wengine ni Viongozi toka Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ), Jeshi la
Polisi, Jeshi la Magereza na wageni waalikwa.
No comments:
Post a Comment