WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wednesday, 24 February 2016

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI, KATIBU MKUU WALA VIAPO KUIONGOZA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akila kiapo cha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akila kiapo cha kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni  mara baada ya kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni kabla ya kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza..
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, mara baada ya Jaji huyo kuwaapisha kuwa viongozi wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza katika tukio lililofanyika Mahakamani hapo, jijini Dar es Salaam leo. Injinia Masauni katika Tume hiyo amekuwa Makamu Mwenyekiti, na Meja Jenerali Rwegasira amekuwa Katibu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a Comment