Mwenyekiti wa
Bodi ya Taifa ya Parole, Jaji Mstaafu Eusebia Munuo (kushoto) akiongoza kikao
cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kuachiliwa kwa Parole. Kulia ni Kaimu
Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole, Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa. Kikao hicho cha siku mbili kimeanza leo Juni 26,
2014 katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli, Jijini Mwanza.
Baadhi ya
Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya
Parole Jaji Mstaafu Eusebia Munuo (hayupo pichani) wakati akitoa hoja ya
kufungua Kikao cha kupitia mapendekezo ya Wafungwa waliopendekezwa kuachiliwa
kwa Parole (wa kwanza kulia) ni Francis Stolla akiwa na Wajumbe wenzake
wakipitia makabrasha ya mapendekezo hayo.
Wajumbe wa
Sekretarieti ya Taifa ya Parole wakifuatilia majadiliano katika Kikao cha Bodi
ya Taifa ya Parole (wa kwanza kulia) ni Afisa Mwandamizi Kitengo cha Parole,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Rose Odemba
wakifuatilia kwa makini majadiliano ya Wafungwa watakaoachiliwa kwa Parole (katikati)
ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole, Mrakibu Msaidizi wa
Magereza, Bruno Pancras (wa kwanza kushoto) ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza,
Merikior Komba.
Wajumbe wa Bodi
ya Taifa ya Parole wakiwasili katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli tayari kwa Kikao
cha Bodi ya Taifa ya Parole kitakachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Juni
26, 2014 katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli, Jijini Mwanza (wa kwanza mbele) ni
Mjumbe wa Bodi, Ayub Mwenda toka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Nchini(kushoto)
ni Jonas Tarimo, Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole toka Ofisi ya Kamishna wa
Ustawi wa Jamii.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Mnuo (kushoto) akifanya
mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari kabla ya kuanza rasmi kwa Kikao cha
Ishirini na Sita cha Bodi ya Taifa ya Parole mapema leo Juni 26, 2014. Kikao
hicho kitafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli, Jijini Mwanza.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment