WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Sunday, 22 June 2014

NAIBU KATIBU MKUU, MKWIZU ALITEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI MAONYESHO YA UTUMISHI WA UMMA DAR


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu (kulia) akimsikiliza kwa makini Afisa Tawala Mwandamizi wa Idara ya Wakimbizi, Jenita Ndone wakati alipokuwa anaeleza majukumu ya Idara hiyo ambayo inasimamia masuala ya wakimbizi nchini, wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Manzi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika Banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni Afisa Habari wa Wizara hiyo, Christina Mwangosi.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Ustawi wa Jamii, Editha Kagaruki wa Idara ya Huduma kwa Jamii, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu akimuuliza swali Stesheni Sajenti Aliko Mwakalindile (kushoto) alipotembelea Banda la Jeshi la Polisi.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu (kulia) akiwa katika Banda la Jeshi la Magereza.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu (wapili kushoto-waliokaa), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga (kushoto-waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment