Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akipokea Salaam ya heshima toka
kwa Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza(hawapo
pichani) katika maadhimisho ya Siku ya Magereza(Magereza Day). Kushoto katika
picha ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja (kulia) ni
Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza,
Erasmus Kundy.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akikagua Gadi ya Wanawake
inayoundwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya
Magereza Day yaliyofanyika leo Juni 20, 2014 katika Viwanja vya Chuo cha
Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Msanii
Nguza Viking anayetumikia Kifungo chake Gerezani akiwa na Bendi ya Wafungwa(anayepiga
gitaa) akiimba Wimbo Maalum kuhusu Urekebishaji wa Wafungwa unavyofanyika
Magerezani(wa pili kulia) ni Jonson Nguza Maarufu kwa jina la Papii Kocha
wakitumbuiza katika Maadhimisho ya Magereza Day yaliyofanyika leo Juni 20, 2014
katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(aliyesimama) akitoa
maelezo mafupi kuhusu Madhumuni ya Maadhimisho ya Siku ya Magereza(Magereza
Day). Maadhimisho haya ya siku ya Magereza yanafanyika hapa nchini kwa mara ya
pili ambapo leo yamefanyika katika Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini
Dar es Salaam(wanne kulia katika vazi la suti nyeusi) ni Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, (wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa
Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi.
Mkuu
wa Kitengo cha Kilimo na Mifugo Ndani ya Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Mlasan Kimaro (wa pili kushoto) akitoa maelezo mafupi
kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (suti nyeusi) kuhusu
uzalishaji wa mafuta ya mawese ambayo hutumika kwa matumizi ya Wafungwa
Magerezani alipotembelea Banda la Kilimo na Mifugo. Wapili kulia kwa Waziri
ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja.
No comments:
Post a Comment