WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 20 June 2014

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MATHIAS CHIKAWE ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA YAKE KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, VIWANJA VYA MANAZI MMOJA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe  akipokea  vijitabu vidogo vinavyoelezea masuala ya utendaji wa polisi  kutoka kwa afisa wa Jeshi la Polisi Christina Mponji wakati Waziri huyo alipotembelea Mabanda ya Wizara yake jana katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam .

Maafisa wa jeshi la Magereza wakifurahia jambo pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe  wakati Waziri huyo alipotembelea Mabanda ya Wizara yakejana  katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Mathew Ikomba akitoa maelezo ya namna Idara hiyo ilivyofanikiwa kutumia teknolojia  mpya  ya utoaji wa vibali vya ukaazi kwa mfumo wa kielectroniki na hivyo kuondokana na mfumo wa awali wa kuandika vibali hivyo kwa mkono,  mbele ya   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe  wakati Waziri huyo alipotembelea Mabanda ya Wizara yake jana katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Laurance Kabigi akimuonesha kifaa cha kuzimia moto Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe  wakati Waziri huyo alipotembelea Mabanda ya Wizara yake jana katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam .
Afisa Habari Mkuu na Msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Thomas Willium wa kwanza kushoto  akitoa maelezo ya namna  Mamlaka hiyo inavyotekeleza zoezi la kuandaa na kutoa vitambulisho vya taifa kwa wananchi wakati Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe  alipotembelea Mabanda ya Wizara yake katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe aliyeketi wa tatu kutoka kushoto , akiwa pamoja na watumishi wa Idara za wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwemo Polisi , Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa baada ya Waziri Chikawe kutembelea mabanda ya wizara yake jana katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, aliyeketi wa pili kutoka kushoto ni Msemaji wa wizara Isaac Nantanga.

No comments:

Post a Comment