WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 17 June 2014

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MABANDA MAONYESHO UTUMISHI WA UMMA DAR


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimsikiliza kwa makini Afisa Tawala Mwandamizi wa Idara ya Wakimbizi, Jenita Ndone wakati alipokuwa anaeleza majukumu ya Idara hiyo ambayo inasimamia masuala ya wakimbizi nchini, wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Manzi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto) akimuuliza maswali Afisa wa Idara ya Uhamiaji, Mathew Ikomba kuhusu matatizo mbalimbali likiwemo baadhi ya wananchi wanailalamikia Idara hiyo kuhusu uombwaji wa rushwa wakati wanapoomba kupatiwa Hati ya Kusafiria (pasipoti). Malemi aliitaka idara hiyo ifuate haki wakati wananchi wanapoomba pasipoti. Wizara na Idara zake inashiriki katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Loyce Abeid, akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto) kifaa kinachotumika kwa ajili ya uokozi wa magari yanapopata ajalia hasa magari ya tenki. Malemi alitetembelea Banda la Wizara na Taasisi zake katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.   Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wapili kulia) katika Banda la Nida kujifunza masuala mbalimbali ya kiutendaji yanayofanywa na Mamlaka hiyo iliyopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Habari wa Wizara hiyo, Christina Mwangosi.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
                                  

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wapili kushoto aliyekaa kwenye kiti) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wizara yake ambao wapo katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kushoto aliyekaa kwenye kiti ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto) akiondoka katika Viwanja vya Mnazi Mmoja baada ya kumaliza kuangalia na kujifunza zaidi shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara yake katika maonyesho hayo yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  

No comments:

Post a Comment