WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 16 June 2014

MKUCHIKA ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA DAR


Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Taasisi zake wakipita kwa maandamano mbele ya Jukwaa Kuu la Mgeni Rasmi ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora, George Mkuchika  wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika (kushoto) alipotembelea Banda la Wizara hiyo wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika (wapili kulia) akitazama moja wapo ya vielelezo vilivyopo katika Banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri Mkuchika alitembelea Banda hilo katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Stesheni Sajenti Aliko Mwakalindile (kushoto) wa Polisi Makao Makuu akiwaonesha beji za vyeo mbalimbali vinavyotumiwa na Jeshi la Polisi wakati wananchi hao walipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
                        
Wanafunzi wakiangalia Bango la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi linaloonesha Viongozi Wakuu wa Wizara hiyo katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Elvis Mlemba (wapili kushoto) akijibu maswali mbalimbali ya mwananchi aliyekuwa anataka kujua kuhusu vifaa vya uzimaji moto na uokoaji. Kulia ni Koplo Loyce Abeid, wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Wananchi wakipita katika Banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kujifunza masuala mbalimbali yanayofanywa na Wizara hiyo na Taasisi zake katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wananchi mbalimbali wakiwa katika Banda la Jeshi la Magereza kujifunza masuala mbalimbali yanayofanywa na Jeshi hilo katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji, Rudovic Kimoro (kulia) akimpa mwananchi kipeperushi kilichoandikwa masuala mbalimbali ya hati ya kusafiria (Pasipoti) wakati mwananchi huyo alipolitembelea Banda la Uhamiaji liliopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment