Ndugu zangu ,
Toka juzi nimeona watu kadhaa wakiponda hatua
ya Idara ya uhamiaji kuita kwenye usaili watu zaidi ya alfu 1 wakati
wanaotakiwa ni watu 70 tu .
Kuna jamaa wamechukulia hili kama ajenda
ya kisiasa na kuanza kuhoji au kurushia vijembe vyama vingine vya kisiasa
kusuatia kadhia hiyo .
Tunachopaswa kujua ni kwamba idara ya
Uhamiaji ni Nyeti kama zilivyo idara nyingine za kiulinzi na usalama nchini ,
mchujo wake unahusisha vitu vingi sana kuliko ilivyo awali , sio elimu tu na
afya tu kuna masuala ya uelewa wa vitu mbalimbali , historia yako ya nyuma ,
mahusiano yako na hata kwenye mafunzo na mazoezi kabla ya kuanza kazi rasmi .
Kwahiyo ukichukuwa watu hao alfu 1 au 2 ,
ukiwaweka kwenye mizani hiyo unaweza kupata hao 70 au usipate kabisa
kutegemeana na vigezo vilivyowekwa na idara yenyewe .
Naipongeza idara kwa hatua yake ya kuwa
wazi kwa kuita watu kwa mkupuo sehemu moja kwa ajili ya usaili , maana pale
msailiwa anaangaliwa toka wakati anaingia uwanjani , atakavyowasiliana na
wenzake na masuala mengine mengi , ndio tupo kwenye dunia hiyo ya kuangaliana
kabla ya majukumu .
Tumeona operesheni ya kuondoa wahamiaji
haramu ilivyoleta madudu mengi nchini mpaka kuundwa kamati na wengine kujiuzuru
, hatupendi hiyo itokee tena ndio maana usaili unatakiwa uwe wa makini , wawazi
na wenye viwango .
Tusipende kuponda na kudharau kila kitu
haswa hivi vinavyohusu usalama wetu wenyewe .
...........................
Yona Fares Maro
No comments:
Post a Comment