WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wednesday 18 June 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WASAILIWA 1,281 KUINGIA DURU YA MWISHO YA USAILI WA NAFASI YA MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WASAILIWA 1,281 KUINGIA DURU YA MWISHO YA USAILI WA NAFASI YA MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI (ASSISTANT INSPECTOR OF IMMIGRATION)

Wasailiwa 1,281 kati ya 6,115 waliofanya usaili wa kwanza tarehe 13 Juni, 2014 jijini Dar es Salam kuomba nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji (Assistant Inspector of Immigration) wanatarajiwa kuingia duru ya pili na ya mwisho ya usaili huo baada ya kufanikiwa kufaulu usaili wa kwanza.
Usaili huu ambao utafanyika kwa awamu utaanza tarehe 23 Juni hadi 03 Julai, 2014 na utafanyikia katika Bwalo la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1.30 asubuhi.
Tofauti na usaili wa kwanza ambao ulikuwa wa kuandika na ulihusisha maswali ya hesabu na ufahamu wa jumla, usaili wa awamu ya pili utakuwa wa maswali ya ana kwa ana ambao utahusisha kupima uwezo wa msailiwa kujieleza na kufafanua mambo.
Kuchaguliwa kwa wasailiwa hawa kulifanyika baada ya kusahihisha majibu yao na majina kuingizwa katika mfumo wa kimtandao ambao ulisaidia kuchagua wasailiwa waliopata alama hamsini na kuendelea.
Majina ya wasailiwa hawa yanapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, www.moha.go.tz  na ya Idara ya Uhamiaji, www.uhamiaji.go.tz na watatakiwa kuja na vyeti vyao halisi vya kuzaliwa, vya shule na picha mbili za pasipoti.
Awali, kiasi cha wasailiwa 10,801 waliitwa kwa ajili ya usaili wa kwanza baada ya kupokea maombi yao, lakini waliohudhuria ni 6,115 na kati yao ndio walipatikana 1,281 ambao watasailiwa ili kupata watakaojaza nafasi sabini (70) za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji katika Idara ya Uhamiaji.

Sgn
Isaac J. Nantanga
0754 484286
MSEMAJI,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
18 Juni, 2013

No comments:

Post a Comment