Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimpa cheti cha uraia wa
Tanzania, Mkimbizi wa Kisomali mwenye asili ya Kibantu, Ramadhani Haji katika
hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Waziri Chikawe alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika Makazi
ya Chogo ambao waliomba kupewa uraia kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania. Kulia
kwa Waziri ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi
(UNHCR), Joyce Mends-Cole na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison
Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na mamia ya wakimbizi wa
Kisomali wenye asili ya Kibantu (hawapo pichani), baada ya kutoa vyeti vya
uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika Makazi ya Chogo, Wilaya ya
Handeni mkoani Tanga. Katika hotuba yake, Waziri Chikawe aliwataka Wakimbizi
hao ambao sasa ni raia halali wa Tanzania kudumisha amani kwa kufuata sheria za
nchi ili waweze kuishi kwa amani. Kulia (Meza Kuu) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
Tanga, Salum Chima. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison
Mseke na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi
(UNHCR), Joyce Mends-Cole. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watatu kulia waliokaa), Kaimu Mkurugenzi
wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (kulia), Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,
Salum Chima (wapili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya Wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu baada ya kupewa vyeti
vya uraia wa Tanzania.Waziri Chikawe alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 1,514
waliopo katika Makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Katika hotuba
yake, Waziri Chikawe aliwataka Wakimbizi hao ambao sasa ni raia halali wa
Tanzania kudumisha amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze kuishi kwa
amani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu
ya Wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu wanaoishi katika Makazi ya Chogo,
Handeni mkoani Tanga wakimshangilia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (hayupo
pichani) alipofika katika makazi yao ili kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania kwa
wakimbizi 1,514 waliopo katika makazi hayo baada ya kuomba uraia kwa mujibu wa
sheria ya Tanzania. Waziri Chikawe alitoa vyeti kwa wakimbizi hao na kuwataka kudumisha
amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze kuishi kwa amani. Picha zote na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA
MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment