WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 28 July 2014

MAJAMBAZI 10 HATARI WAKAMATWA NA SILAHA/BUNDUKI NANE MMOJA MWANAMKE ANAYEJUA KUTUMIA SMG                                  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

 PRESS RELEASE
28/07/2014

MAJAMBAZI 10 HATARI WAKAMATWA NA SILAHA/BUNDUKI NANE MMOJA MWANAMKE ANAYEJUA KUTUMIA SMG

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata mtandao hatari a majambazi wapatao kumi (10) mmoja wao akiwa ni mwanamke anayeshiriki kikamilifu wakati wa matukio ya ujambazi.  Majambazi hao wamekamatwa katika msako mkali unaoendelea jijini D’Salaam katika harakati za kuhakikisha kwamba maisha na mali za wakazi wa D’Salaam vinalindwa kikamilifu.  Katika msako huo watuhumiwa walipekuliwa katika miili, makazi, na maficho yao na wakakamatwa na jumla ya silaha 8 kama ifuatavyo.
1.    SMG NO. 13975 ikiwa na risasi 11 na magazine 2
2.    SMG 1 haikuwa na magazine na namba hazisomeki.
3.    BASTOLA 1 aina ya LUGER yenye namba 5533K
4.    BASTOLA 1 aina ya BROWNING yenye namba TZACR83494 S/No.7670
Na risasi 6 ndani ya magazine.
5.    S/GUN PUMP ACTION na risasi 55
6.    MARCK IV iliyokatwa mtutu na kitako yenye magazine 1 na risasi 4
7.    BASTOLA 1 yenye namba A963858 browning ambayo ina risasi 1
8.    SMG 1 ambayo iko kwa mtaalam wa uchunguzi wa silaha (Balistic)
9.    SHOT GUN TZ CAR 86192 ilitelekezwa baada ya msako
     
S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment