WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 4 August 2014

CHIKAWE AWAAPISHA WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA TUME YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimuapisha Afisa Utumishi wa wizara hiyo, Anna Yusufu Mariam  kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa askari wa majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimpa hati ya kiapo Afisa wa Jeshi la Polisi, Jonas Mugendi baada ya kumuapisha kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na katikati ni Katibu Mkuu, Mbarak Abdulwakil. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto-meza kuu) akiongoza kikao cha Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya kiutumishi na kiutendaji wa askari katika Majeshi hayo, katika  Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nda ni ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kulia Meza Kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment