WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 4 August 2014

BALOZI WA UJERUMANI NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE D’SALAAM

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke alipokuwa akimfafanulia jambo wakati Balozi huyo na Naibu wake walipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ujerumani na Tanzania. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimfafanulia jambo Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke wakati Balozi huyo na Naibu wake, John Reyels (kulia) walipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ujerumani na Tanzania. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiagana na Naibu Balozi wa Ujerumani nchini, John Reyels wakati Naibu huyo na Balozi wake, Egon Kochanke (katikati) walipomaliza mazungumzo na Waziri Chikawe ofisini kwake Dar es Salaam baada ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ubalozi huo na Wizara yake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment