JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI
LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
04/08/2014
ASKARI
POLISI FEKI WA USALAMA BARABARANI ALIYEKUWA ANATAPELI WANANCHI AKAMATWA JIJINI
DAR ES SALAAM
Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es
Salaam linamshikilia na kumhoji mtu mmoja aitwaye ROBSON S/O SEIF MWAKYUSA
EMMANUEL, miaka 30, Mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za
kujifanya afisa wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani akiendelea na kazi za
ukaguzi wa makosa ya usalama barabarani. Mtuhumiwa huyu alikamatwa tarehe
02/08/2014 huko Kata ya Chamazi, Mbagala Majimatitu Mkoa wa Kipolisi Temeke akiwa
amevalia sare za Polisi na cheo cha Stesheni Sajenti.
Baada ya kukamatwa alikutwa
na gari namba T723 BAK T/Cresta rangi nyeupe analilotumia kuzunguka maeneo
mbalimbali ya jiji kutapeli watu akiwadanganya yeye ni askari polisi. Gari hilo
lilipopekuliwa lilikutwa na
·
Radio
Call 1yenye namba GP380 aina ya Motorola
·
Leseni
za udereva zipatazo 40 za watu mbalimbali
·
Stakabadhi
02 za Serikali zenye nambari A0531562 na A1672464
·
Police
Loss Report mbalimbali.
·
Nakala
03 za Notification zilizojazwa.
·
Kofia
moja ya (Uhuru Cape) ya Usalama barabarani,
·
Beji
01 yenye jina la E.R. MWAKYUSA ya kuweka kifuani.
·
Ratiba
ya mabasi yaendayo Mikoani ya SUMATRA
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment