Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimsikiliza kwa makini Askofu
Kiongozi wa Kanisa la Moravian nchini, Alinikisa Cheyo (wapili kushoto) wakati
wa mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe jijini Dar es Salaam
leo. Maaskofu watano wa Kanisa hilo ambalo limekumbwa na mgogoro kwa muda mrefu
sasa walionana na Waziri huyo ili kuomba msaada wake katika kudhibiti vurugu zinazoendelea
katika Kanisa hilo. Hata hivyo, Waziri Chikawe aliahidi kulifanyia kazi na
hatimaye kulitolea maamuzi suala hilo baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa
kukutana na pande zote mbili zinazogombana. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Maaskofu
wa Kanisa la Moravian nchini baada ya
kuwasikiliza malalamiko yao kuhusiana na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe
inayoendelea kwa muda mrefu katika Kanisa hilo. Maaskofu hao ambao walikuwa
wanaongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Alinikisa Cheyo walimuomba Waziri
Chikawe aingilie kati kwa kudhibiti vurugu hizo ambazo zinazisambaratisha
kanisa lao. Hata hivyo, Waziri Chikawe aliahidi kulifanyia kazi suala hilo na
atalitolea maamuzi baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa kukutana na pande
zote mbili zinazogombana. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimsikiliza kwa makini
Askofu wa Kanisa la Moravian nchini, Conrad Nguvumali (watatu kulia) wakati wa
mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe jijini Dar es Salaam
leo. Maaskofu watano wa Kanisa hilo ambalo limekumbwa na mgogoro kwa muda mrefu
sasa, wakiongozwa na Askofu Kiongozi wa Kanisa hilo nchini, Alinikisa Cheyo
(wapili kushoto) walionana na Waziri huyo ili kuomba msaada wake katika
kudhibiti vurugu zinazoendelea katika Kanisa hilo. Hata hivyo, Waziri Chikawe
aliahidi kulifanyia kazi na hatimaye kulitolea maamuzi suala hilo baada ya
kufanya uchunguzi wa kina kwa kukutana na pande zote mbili zinazogombana. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment