WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 11 August 2014

JESHI LA MAGEREZA LAIBUKA MSHINDI WA PILI WA JUMLA KITAIFA, MKOANI LINDI


Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro(kulia) akimuongoza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Ghalib Bilal(kushoto) alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza leo Agosti 08, 2014 katika Kilele cha Maonesho ya Nane Nane, Ngongo Mkoani Lindi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Ghalib Bilal akiangalia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza kupitia Kiwanda chake cha Gereza Karanga, Moshi alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza katika Kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa, Mkoani Lindi(kulia) ni Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mlasani Kimaro.


Mtaalam wa Mifugo(Ndege) Sajini Taji wa Magereza Nesia Hozza(kushoto) akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Ghalib Bilal juu ya namna ya Ufugaji wa Kuku unavyoweza kuongeza kipato kwa Wananchi wa kawaida alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza katika Kilele cha Maonesho ya Nane Nane, Mkoani Lindi.

Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza walioshiriki Maonesho ya Nane Nane Kitaifa, Mkoani Lindi wakifurahia ushindi wa Pili wa jumla katika Kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa yaliyofanyika Mkoani Lindi.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Ghalib Bilal akikabidhi zawadi kwa Mshindi wa Pili wa Jumla Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro katika Kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa yalifungwa leo rasmi Agosti 08, 2014 katika Viwanja vya Ngongo, Mkoani Lindi.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment