WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Sunday, 20 July 2014

WAZIRI CHIKAWE ASHIRIKI MAZISHI YA MZAZI WA DIWANI NACHINGWEA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) na waombolezaji wakiswalia mwili wa marehemu ambaye ni mama mzazi wa Diwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea,  Sada Makota. Mazishi ya Mama Mzazi wa Diwani huyo yamefanyika katika Kijiji cha Nangunde, Kata ya Namikango wilayani Nachingwea leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kulia) akimfariji Diwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Sada Makota kwa kufiwa na mama yake mzazi, wakati alipofika nyumbani kwa Diwani huyo wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika katika Kijiji cha Nangunde, Kata ya Namikango wilayani Nachingwea leo.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya Mama Mzazi wa Diwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Sada Makota, wakati alipofika nyumbani kwa Diwani huyo katika Kijiji cha Nangunde, Kata ya Namikango wilayani Nachingwea leo.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (aliyevaa Miwani) akiwa na waombolezaji wa msiba wa Mama Mzazi wa Diwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Sada Makota. Mazishi ya Mama Mzazi wa Diwani huyo yamefanyika katika Kijiji cha Nangunde, Kata ya Namikango wilayani Nachingwea leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment