Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na maelfu ya Waumini wa Karismatiki
Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea
Taifa yaliyofanyika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo aliyataka Makanisa
nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na kuepuka kuingia
katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu
amani makanisani. Aidha, Chikawe aliongeza kuwa migogoro katika Makanisa na Madhehebu
mbalimbali nchini imekuwa mingi katika kipindi hiki ambapo migogoro hiyo
inasababishwa na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa mali
za Kanisa. Kutokana na migogoro hiyo Chikawe alisema “Serikali haitavumilia
vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani na ikibidi itafuta usajili wa
madhehebu na makanisa yenye migogoro ili kuepusha shari”. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akiungana na maelfu ya Waumini
wa Karismatiki
Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea
Taifa. Mapombi hayo yalifanyika katika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar
es Salaam leo. Waziri Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo
aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea
Taifa na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa
kuingia katika uvunjifu amani makanisani. Aidha, Chikawe aliongeza kuwa
migogoro katika Makanisa na Madhehebu mbalimbali nchini imekuwa mingi katika
kipindi hiki ambapo migogoro hiyo inasababishwa na ubinafsi wa viongozi,
kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa mali za Kanisa. Kutokana na migogoro hiyo
Chikawe alisema “Serikali haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani
na ikibidi itafuta usajili wa madhehebu na makanisa yenye migogoro ili kuepusha
shari”. Picha na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment