WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Thursday 28 August 2014

BALOZI WA CHINA NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE DAR

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akizungumza na Balozi wa China nchini, Lu Youqing (watatu kulia) pamoja na maafisa wa ubalozi huo, masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo.
Balozi wa China nchini, Lu Youqing (wapili kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) wakati balozi huyo pamoja na maafisa wake walipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment