WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday 12 August 2014

VODACOM YAMKABIDHI WAZIRI CHIKAWE MAMILIONI KWA AJILI YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI ITAKAYOFANYIKA JIJINI ARUSHA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akimshukuru Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (kushoto) baada ya kupokea hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 40 msaada uliotolewa kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, jijini Arusha. Wapili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, na kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kupokea hundi ya Sh. Milioni  kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, kutoka kwa Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (watatu kulia). Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani  inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, jijini Arusha. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Wapili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:

Post a Comment