Mwenyekiti
wa Kamati Maalumu ya Kuhoji Waomba Hifadhi (NEC), Faraja Nchimbi (watatu
kushoto), Katibu wa Kamati hiyo, Philo Nombo (watatu kulia) ambaye anamwakilisha
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe
wa Kamati hiyo baada ya kuwahoji waomba hifadhi katika Kambi ya Wakimbizi ya
Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Waombaji hao wanatoka nchi
mbalimbali ambapo wengi wao wanatoka nchini Kongo. Zaidi ya waomba hifadhi 300 wanaendelea kuhojiwa na Kamati hiyo
ambayo inaongozwa na Taasisi nane za Serikali ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashtaka ya Jinai (DPP), Idara ya Wakimbizi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Ofisi ya Inspekta Jererali wa Polisi, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na
Shirika la Kimataifa ya Kuhudumia Wakimbizi ambao ni waangalizi wa tukio hilo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
|
No comments:
Post a Comment