|
Mratibu wa Idara ya Wakimbizi
Kanda ya Kigoma, Tony Laiser akiwaongoza Wakimbizi wazee kutoka nchini Kongo leo
kufanyiwa uhakiki wa taarifa zao ili watambulike rasmi kuwa ni wakimbizi katika
Kambi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Zaidi ya familia za
Wakimbizi 14,000 ikiwa ni sawa na Wakimbizi 68,000 wamefanyiwa uhakiki huo
kambini hapo.
|
|
Mratibu wa Idara ya Wakimbizi
Kanda ya Kigoma, Tony Laiser (kulia) akimuhoji Mkimbizi kutoka nchini Burundi,
Bibi Karumere (katikati) wakati wa kufanyiwa uhakiki wa taarifa zake ili aweze kutambulika rasmi kuwa ni Mkimbizi
katika Kambi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Zaidi ya familia
ya Wakimbizi 14,000 sawa na jumla ya Wakimbizi 68,000 wamefanyiwa uhakiki huo
kambini hapo.
|
Mratibu wa Idara ya Wakimbizi
Kanda ya Kigoma, Tony Laiser (kulia) akimkabidhi Mkimbizi kutoka nchini Kongo
katika Kambi ya Nyarugusu msaada wa taa inayotumia mionzi ya jua. Taa hiyo pia
ina sehemu ya kuchajia simu za mikononi. Maelfu ya wakimbizi katika Kambi hiyo walipewa
msaada huo leo ulitolewa na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani
(UNHCR) kupitia Shirika linalotoa huduma za Kijami na Unyanyasaji wa Kijinsia (IRC)
ikiwa ni kawaida yao kutoa misaada mbalimbali ya kuwasaidia wakimbizi hao
waliopo katika kambi hiyo, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
|
Mama Mkimbizi kutoka nchini Kongo
akiwa na mwanae, pamoja na wakimbizi wengine wakisubiria kwenda kufanyiwa
uhakiki wa taarifa zao leo ili waweze kutambulika rasmi kuwa ni wakimbizi
katika Kambi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Zaidi ya familia
ya Wakimbizi 14,000 sawa na jumla ya Wakimbizi 68,000 wamefanyiwa uhakiki huo
kambini hapo. Picha zote na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
|
No comments:
Post a Comment