WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wednesday 17 September 2014

KAMPUNI YA PUMA ENERGY YAMKABIDHI SILIMA MAMILIONI YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI ITAKAYOFANYIKA WIKI IJAYO JIJINI ARUSHA


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy nchini, Philippe Corsaletti (kulia) baada ya kupokea hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 40 msaada uliotolewa kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo, jijini Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ukumbi mdogo wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea hundi ya Sh. Milioni 40 kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy nchini, Philippe Corsaletti (kulia). Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inatarajiwa kufanyika wiki ijayo, jijini Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ukumbi mdogo wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment