WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 22 September 2014

MKUU WA MKOA ARUSHA AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA JIJINI ARUSHA LEO

Washiriki wa maonesho, wananchi mbalimbali wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Kiwanja cha Mpira wa Amri Abeid jijini Arusha leo. Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo aliyazindua maonesho hayo huku akiwataka madereva nchini wawe makini kwa kufuatia sheria za barabarani ili kuepuka ajali. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa jijini Arusha  leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”. Katika hotuba yake, Mrongo aliwataka viongozi wa usalama barabarani kuhakikisha kuwa adhabu dhidi ya madereva wazembe nchini inaongezeka ili wawe na woga wa kufanya makosa barabarani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kushoto) akimpa zawadi ya ngao Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo baada ya mgeni rasmi huyo kuyafungua Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo kitaifa yanafanya jijini Arusha. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
Waendesha pikipiki (bodaboda) pia walishiriki kikamilifu katika uzinduzi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Kiwanja cha Mpira cha Amri Abeid, jijini Arusha leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”. 
Trafiki Makao Makuu jijini Dar es salaam, Mkaguzi Msaidizi, Yohana Mjema (kulia), akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo (watatu kushoto), namna ajali barabarani zinavyoweza kuepukika endapo watumiaji barabara watakuwa waangalifu kwa kufuata sheria za barabarani. Mkuu wa Mkoa aliyazindua maonesho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani katika Kiwanja cha Mpira Amri Abeid jijini Arusha leo. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mohamedi Mpinga.
Sajenti wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Damian Muheya (kulia) akiwaelimisha wananchi wa jijini Arusha jinsi mtungi mdogo wa kuzimia moto unavyotumika wakati moto unapotokea. Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani imezindulia leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (Magesa Mrongo katika Kiwanja cha Mpira cha Amri Abeid jijini humo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo (katikati waliokaa), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wanne kutoka kushoto-waliokaa) wakiwa na wajumbe wa usalama barabarani katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo Kitaifa mwaka huu yanafanyika jiijini Arusha leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment