Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani,
Pereira Ame Silima akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao
unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini.
Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi
Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga. Kulia ni Mwenyekiti wa Mafunzo na
Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho
ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose
jijini Arusha leo.
|
No comments:
Post a Comment