WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday 1 December 2014

PICHA MBALIMBALI ZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KILICHOFANYIKA JIJINI ARUSHA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Mbarak Abdulwakil    wa pili kutoka kushoto akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw.Adoh Mapunda muda mfupi kabla ya Bw. Mapunda kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kilichoanza leo jijini Arusha katika hoteli ya Corridor Springs.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Mbarak Abdulwakil wa tatu kutoka kulia akimkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha  Bw. Adoh  Mapunda kwenda kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kilichoanza leo jijini Arusha katika hoteli ya Corridor Springs, wa kwanza kutoka kulia ni Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahman Kaniki anayefuatia ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Sylivester Ambokile.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha  Bw. Adoh Mapunda  wa kwanza kutoka kulia akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Mbarak Abdulwakil   baada ya Bw. Mapunda kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kilichoanza leo jijini Arusha katika hoteli ya Corridor Springs.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Mbarak Abdulwakil    wa pili  kutoka kulia akiimba wimbo wa Solidarity  Forever pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wa pili kutoka kulia ni Katibu wa Baraza hilo la Wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Mbarak Abdulwakil    wa pili  kutoka kulia akiimba wimbo wa Solidarity  Forever pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wa pili kutoka kulia ni Katibu wa Baraza hilo la Wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Jenitha Ndone.Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi limeanza  leo jijini Arusha katika hoteli ya Corridor Springs.
Sehemu ya wajumbe na wakuu wa Idara mbalimbali za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi waliohudhuria kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  katika picha ya pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw.Adoh Mapunda muda mfupi baada  Bw. Mapunda kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kilichoanza leo jijini Arusha katika hoteli ya Corridor Springs.
Bw. Peter Mbelwa  kutoka Mamlaka ya Kudhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) akitoa mada kuhusu Maandalizi ya kustaafu katika kikao cha  Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kinachoendelea jijini Arusha katika hoteli ya Corridor Springs.                                                    
Sehemu ya wajumbe wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakishiriki kikao hicho  kinachoendelea jijini Arusha katika hoteli ya Corridor Springs, wa kwanza  kutoka kushoto ni Avelin Momburi ambaye ni  Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).


No comments:

Post a Comment