WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday 2 March 2015

TAMASHA KUBWA LA MICHEZO LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI NA TAASISI ZAKE LAFANYIKA, LAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (kushoto) akimsalimia mtumishi wa Wizara hiyo, Said Ngovi ambaye ni mvuta kamba wa timu ya Utawala wakati Mkurugenzi huyo alipokuwa anazikagua timu mbalimbali za wizara hiyo katika Tamasha la Michezo la kwanza lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kapteni wa timu ya wanaume (Utawala) ya kuvuta kamba, Ally Lubuva.
Kapteni wa Timu ya Utawala ya kuvuta kamba wanaume, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Neema Chilipweli (kushoto) akiimasisha timu yake kuivuta timu ya Uhamiaji (haipo pichani) wakati timu hizo zilipokuwa zikishindana katika Tamasha kubwa la Michezo lililoandaliwa na wizara hiyo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi wake na kuwawezesha kufanya mazoezi ya viungo. Tamasha hilo ambalo la kwanza kufanywa na wizara hiyo lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mary Nyegazeni akiishangilia timu yake ya Utawala ya kuvuta kamba wanaume baada ya kunyakua pointi mbili kwa kuivuta timu ya Uhamiaji katika mashindano maalumu ya Tamasha la Michezo la wizara hiyo ambalo lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
Mtumishi wa Idara ya Uhamiaji, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Amina Mavengero (katikati) akicheka kwa furaha baada ya kushinda mchezo wa kufukuza kuku kwa kuwapiku wenzake wa Timu ya Utawala, Mary Nyegazeni (kushoto) na Consalva Nagamchonga wa Timu ya Jeshi la Magereza. Mchezo huo ulishirikisha watumishi wenye umri zaidi ya miaka 55 katika timu zote zilizoshiriki.  Wizara hiyo pamoja na Taasisi zake za Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zilifanya mashindano ya michezo mbalimbali yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam leo, ambapo Tamasha hilo lilifunguliwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lilian Mapfa.
Timu ya Utawala ya kuvuta kamba wanawake, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiivuta timu ya Uhamiaji (haipo pichani) wakati timu hizo zilipokuwa zikishindana katika Tamasha kubwa la Michezo lililoandaliwa na wizara hiyo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi wake na kuwawezesha kufanya mazoezi ya viungo. Tamasha hilo ambalo la kwanza kufanywa na wizara hiyo lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akizungumza na wanamichezo wa timu za Utawala, Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) walioshiriki katika michezo ya Kuvuta kamba, mpira wa miguu, riadha, Netiboli na kufukuza kuku katika Tamasha kubwa la Michezo lililoandaliwa na Wizara hiyo kwa ajili ya kuwakutanisha watumishi wake na kuwawezesha kufanya mazoezi ya viungo. Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Probesheni na Huduma kwa Jamii, Fidelis Mboya, na kulia ni Jesuad Ikonko, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (kushoto), Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa (wapili kushoto) wakijumuika kulisakata rumba na wanamichezo wa Wizara na Taasisi zake katika Tamasha la Michezo la kwanza lililofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam leo. Tamasha hilo lilijumuisha timu za Utawala, Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida).
Katibu wa Michezo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jarahi Kilemile akimshukuru Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (hayupo pichani) kwa kulifungua na kufunga Tamasha kubwa la michezo la wizara hiyo lililofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam leo. Tamasha hilo lilijumuisha timu za Utawala, Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a Comment